OWNER AT WORK

OWNER AT WORK
BLOGGER

ABCD OPEN SOURCE LIBRARY SOFWARE

Wapendwa habari! Hili tangazo ni kwa mtu yoyote , taasisi, mashirika kwa wanaohitaji ushauri au maonyesho (Demo) na hata kufungiwa ABCD OPEN SOURCE LIBRARY SOFWARE kwa matumizi ya kila siku ndani ya maktaba zetu.

ABCD OPEN SOURCE NI NINI? 

ABCD ni jina. kama ilivyo majina mengine ya library  software. Hivyo KOHA, MANDARIN AU ADLIB HAYA YOTE NI MAJINA YA AINA ZA LIBRARY SOFTWARE.


LIBRARY SOFTWARE NI NINI? kila maktaba ili kutimiza majukumu yake ni lazima kuwe na vitendea kazi hivyo library software zimetengengezwa ili kusaidi kuunganisha shughuli zote za maktaba kufanya kazi kwa pamoja na kwa halaka zaidi.

Ni kazi zipi zinazofanywa na library sofware? Hapa sasa inategemea na uhitaji wa maktaba na aina ya software. Maana kila taasisi au shirika yana manitaji tofauti. Hivyo wanapofunga hizi software wanachagua aina za modules ambazo wanazohitaji kulingana na mahitaji yao. Na modules ni nini? ni zile shughuli kama vile cataloging, circulation, authorities, serials na zingine nyingi. Hivyo muunganiko wa hizi shughuli zinapatikana kwenye package moja ambayo tunaita library software.

Kuna aina kuu mbili za library software kuna za bure (Open SOrce) na zakulipia (commercial) zote zinatimiza majukumu yake sawa hakuna tofauti.
ABCD OPEN SOURCE ni software ya bure ambayo inafanya kazi bila malipo yoyote na gharama zozote. Hivyo inakuwezesha kuwa na ABCD OPAC na ABCD STAFF INTERFACE. Kinachohitajika ni kufanya installation na kupata ushauri wa jinsi ya kuifanyia kazi ili iweze kuperform well.

Mfano hii ni  ABCD STAFF INTERFACE ambayo tunaweza kudesign vyovyote kulingana na mahitaji yako karibuni sana.