Je huwa unasave password yako kwenye browser kama vile mozila firefox, safari, opera, chrome, Internet explorer na nyingine nyingi pale unapo login? Kama ndiyo basi upo kwenye hatari kubwa kwa sababu password hizo ni rahisi kwa mtu kuziona akiwa na computer yako. Tutaangalia Mozila firefox jinsi ambavyo mtu anaweza kuona password zilizohifadhiwa kiurahisi.
1.Juu kabisa kwenye browser yako bonyeza firefox ->open menu na kisha chagua Options
2.Window mpya itafunguka kisha utachagua Security pane, kisha angalia chini na ubonyeze Saved logins
3. Window mpya itafunguka kisha chagua Show Password
